Brendan RodgersBaada ya kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Aresnal jana meneja mkuu wa timu ya Liverpool, Brendan Rodgers ana mpango wa kuwakimbilia Didier Drogba na Michael Owen ili kuongeza makali ya safu yake ya ushambuliaji iliyoanza ligi kwa kusuasua.

Hali hiyo imechangiwa zaidi mara baada ya timu hiyo kubakiwa na washambuliaji wachache baada ya kumuuza Andy Caroll kwa West Ham United., uwezekano wa kumpata Drogba ni mkubwa kutokana na mchezaji huyo kuwa huru kwa sasa mara baada ya timu yake Shanghai Shenhua kumuacha rasmi jana na Owen kwa sasa ni mchezaji huru na kuwasajili kwa sasa pia inawezekana kwa sababu hawana timu zozote kwa sasa.

Tatizo pekee linaloweza kuikabilia Liverpool kushindwa kumsajili Drogba kwa sasa ni mshahara mkubwa itakayolazimika kumlipa mchezaji huo.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.