Chama
Cha Mapinduzi nchini Uingereza jana kilisuka upya safu yake ya uongozi
kwa kuchagua viongozi wapya na kuongeza nafasi mpya za manaibu katika
Sekretarieti ili kuboresha utendaji. Aidha kikao kilikaa kwa utaratibu
maalum na kuridhia kwa pamoja kuongeza nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa
Tawi kutoka Zanzibar.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Tawi ilijazwa na Ndugu Sukwa Said Sukwa aliyepita bila kupingwa ili kuleta uwiano wa kitaifa.
Safu mpya za uongozi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi UK na miji watokayo kwenye mabano ni kama ifuatavyo:
1.0 Katibu wa CCM wa Tawi ni Bi. Mariam Mungula. (East London)
1.1.Naibu Katibu wa CCM Tawi ni Ndugu Albert Ntemi. (Luton)
2.0 Katibu wa Siasa na Uenezi Tawi ni Ndugu Leybab Mdegela (Northampton)
2.1 Naibu Katibu wa Siasa na uenezi Tawi ni Ndugu Abraham Sangiwa (Luton)
3.0 Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi ni Ndugu John Lyimo (Manchester)
3.1 Naibu Katibu wa Uchumi na Fedha ni Ndugu Mohamed Upete (Reading)

4. Kikao hicho vilevile kilimteua Ndugu Haruna Mbeyu maarufu kama “Meya wa London” kuchukua wadhifa wa kuwa “Mshauri Maalum” au “Special Advisor” wa Tawi La Uingereza kutokana na mchango wake mkubwa kwa Watanzania UK.
Kikao kiliridhia pingamizi lililowekwa na wengi wa wajumbe kwa Ndugu Moses Katega kutetea nafasi yake ya Katibu wa Siasa na Uenezi kwa kuzingitia sifa, maadili na miiko ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi itaendelea kuwa na Viongozi wa Tawi na Wenyeviti wa mashina. Aidha Kamati ya Usalama na Maadili sasa itakuwa na wajumbe wafuatao:
- Lilian Barongo - Mwenyekiti.
- Mashamba Mashaka
- Kapinga Kangoma
- Frank Mukiza
- Victor Mgoya
- Joseph Gobbos
Kabla ya uchaguzi ambao uliendeshwa kwa demokrasia ya hali ya juu, Mwenyekiti wa Tawi Ndugu Maina Owino aliwaasa wajumbe kuzingatia haki na wajibu wa uwanachama na sifa na miiko ya uongozi kama ilivyoainishwa katika miongozo na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.
Kikao kilipokea taarifa muhimu ya Kamati Maalum, kilibariki marekebisho ya mwisho ya Website ya kisasa ya CCM UK na kilipitisha mipango mipya ya kuendeleza Chama kwa manufaa ya Watanzania na Wanadiaspora.
Mariam Mungula
Katibu wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi, Uingereza
CHAMA CHA MAPINDUZI -UK.
Imetolewa na Idara ya Siasa na Uenezi, Tawi la CCM ,Uingereza.
Tarehe : 02 Septemba 2012.
Source: wavuti
Post a Comment