|
Mwalimu wa
Ujasiriamali kutoka katika Taasisi ya RafikiElimu Foundation,
Mama Ashankira Lupembe , akifundisha kwa vitendo namna ya
kutengeneza sabuni ya maji. | |
|
Mwanafunzi wa
ujasiriamali akitengeneza sabuni ya unga mwenyewe mara baada ya
kupata maelekezo kutoka kwa waalimu wa ujasiriamali kutoka
RafikiELIMU Foundation. | |
|
Mwanafunzi wa
ujasiriamali akitengeneza sabuni ya maji kwa vitendo mara
baada ya kupata maelekezo kutoka kwa waalimu wa Ujasiriamali
kutoka katika Asasi ya RafikiElimu Foundation. | |
|
Wajasiriamali
wakifanya " practical " ya kutengeneza sabuni ya maji kwa
vitendo mara baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa waalimu wa
ujasiriamali kutoka katika Asasi ya RafikiElimu Foundation. |
|
|
Mwalimu wa
Ujasiriamali kutoka Taasisi ya RafikiElimu Foundation, Mama
Hellen Mbise akielekeza kwa vitendo namna ya kutengeneza
sabuni za maji. |
|
|
Mwalimu
Ashankira Lupembe akiwaonyesha wanamfunzo kitambaa kilcho fuliwa
kwa kutumia sabuni aliyo itengeneza mwenyewe wakati wa
uzinduzi wa EUMIVI PROJECT. |
|
|
Mwalimu wa
Ujasiriamali kutoka Taasisi ya RafikiElimu Foundation, Mama
Ashankira Lupembe akifua kitambaa kwa kutumia sabuni iliyo
tengenezwa wakati wa mafunzo ya utengenezaji sabuni ya wakati
katika uzinduzi wa mradi wa Elimu ya Ujasiriamali Mijini &
Vijijini. | |
|
Mama Ashankira
Lupembe, Mtaalamu na Mwalimu wa Ujasiriamali kutoka RafikiElimu
Foundation akitoa maelekezo ya namna ya kutengeneza sabuni ya
maji kwa vitendo. |
|
Mradi uliolenga kupunguza tatizo la ajira nchini
kwa kutroa elimu ya ujasiriamali kwa maelfu vijana wa
kitanzania waishio mijini na vijijini ifikapo mwezi Novemba
2014 umezinduliwa rasmi leo jijini Dar Es salaam. Uzinduzi
huo ulio fanyika mapema leo katika eneo la Shule Ya Msingi
Mlimani iliyopo katika Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam na
kuhudhuriwa na makumi ya vijana wa kada mbalimbali jijini Dar
es salaam uliambatana na mafunzo ya ujasiriamali ambapo
wahudhuriaji walipata nafasi ya kujifunza kutengeneza sabuni za
aina mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa kutoka katika taasisi
ya RafikiElimu Foundation, taasisi inayo jihusisha na maendeleo
ya jamii.
|
Baadhi ya
wajasiriamali walio hudhuria katika Uzinduzi wa Mradi wa Elimu
Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini uliofanyika leo jijini
Dar Es salaam. |
|
Akiulezea mradi huu, mratibu msaidizi wa mradi
huo alisema kuwa mradi huu upo katika awamu kuu mbili.
Awamu ya kwanza itafanyika kuanzia tarehe
01 Septemba 2012 hadi tarehe 29
Septemba 2012, na utafanyika katika mikoa ya
Dar Es salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Dodoma na Kilimanjaro,
ambapo mbali na kutoa mafunzo ya ujasiriamali, asasi itatafuta
vijana kumi na wawili kutoka katika hiyo mikoa saba kwa
ajili ya kufanya kazi kama wajitoleaji " volunteers" katika
awamu ya pili ya mradi itakayo anza rasmi tarehe 01 Novemba
2012 na kuchukua miaka miwili hadi Novemba 2014 ambapo
ndipo itakapo kuwa tamati ya mradi huu.
Awamu ya kwanza ya mradi huu inafanyika katika mikoa ya Dar
Es salaam, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Dodoma, Mwanza na Mbeya.
Jijini Dar Es salaam, mafunzo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia
tarehe 01 Septemba 2012 hadi tarehe 04 Septemba 2012 katika
Shule ya Msingi Mlimani , iliyopo katika Chuo Kikuu Cha Dar
Es salaam... Ratiba kamili ya awamu ya kwanza ya mafunzo haya
ni kama ifuatavyo :
1. ARUSHA, MOSHI & MOROGORO : Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe
17 hadi 19 Septemba 2012.. Mwisho wa kujiandikisha katika " programme hii " kwa wakaazi wa ARUSHA, MOSHI na MOROGORO ni tarehe
15 Septemba 2012.
|
Baadhi ya wanafunzi wa ujasiriamali waliohudhuria katika mafunzo haya wakifuatilia darasa kwa makini. |
|
2.
MWANZA, MBEYA & DODOMA : Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Septemba 2012.
Mwisho wa kujiandikisha katika programme hii kwa wakaazi wa DODOMA, MBEYA & MWANZA ni tarehe
25 Septemba 2012.
Post a Comment