KATIBU Mkuu wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mohamed Muya, amesema ushirikishwaji wa Mtandao wa Kilimo, Sera na uchambuzi wa Rasilimali za Asili (FANRPAM), ni muhimu kwa sababu utasaidia kuleta kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo kwa wakulima wadogo.
Akizunguza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu semini ya siku saba katika kujadili maendeleo ya kilimo iliyoandaliwa na mtandao huo, kushirikisha washiriki kutoka nchi zaidi ya tano, Muya alisema iwapo mipango hiyo, itasimamiwa vizuri hakika mafanikio yatapatikana.
Alisema ushirikishwaji wa mtandao huo, utasaidia kuwapatia wakulima nyenzo mbalimbali za klimo pembeje ambazo zitawasaidia kuzalisha mazao kwa waingi ikiwamo ya biashara kwa lengo la kujiongezea kipato.
“Kushirikiana na watu kama hawa ni muhimu sana kwa sababu hukuna hata mtu anaweza kujiletea maendeleo yake binafsi pamoja na bila kushirikiana na watu wengine wenye mtazamo wa kimaendeleo.”alisema Muya.
Naye mtoa mada kwenye semina hiyo, Dk Sepo alisema wanapozungumzia mabadiliko ya tabianchi ni kwamba wanazungumzia athari zake kuhusu sekta zote kuhusu maisha ya jamii kwa ujumla wake.
Alisema kutokana na kutambua hilo ndiyo maana FANRPAN ikaamua kuunga na kushirikiana na serikali , wadau wa kilimo pamoja na sekta binafsi kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wadogowadogo ili waweze kujikomboa kamaendeleo.
Alitoa wito kwa wakulima wa maeneo ambayo hayana mvua za kutosha kujitahidi kulima mazao yanayostahimili ukame.
Mwisho
Mwandishi wetu
Post a Comment