- Simu kuuzwa kwa shilingi 74,999, wateja kupata huduma ya facebook, twitter na Wikipedia bure.
- Simu ina kadi yenye uwezo wa GB 32 wa kutunza kumbukumbu na Kamera.
Dar es Salaam, 5 Septemba, 2012 … Watuamiaji wa simu za mkononi sasa wanayo sababu ya kutabasamu, kufuatia kuzinduliwa kwa simu mpya aina ya Nokia 111.
Uzinduzi huo uliofanywa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Nokia na Vodacom Tanzania, umekuja ikiwa ni miezi miwili tangu kuzinduliwa kwa ofa nyingine ya nokia Asha 302, na Nokia Asha 200 kuingizwa katika soko la Tanzania. Simu hiyo itauzwa kwa shilingi 74,999.
Baada ya kununua simu ya Nokia 111, mteja atapata huduma ya intaneti bure na muda wa maongezi mara mbili ya ule atakaonunua kila mwezi kuanzia shilingi 1000/= au zaidi. kwa miezi sita mfululizo.
“Wateja pia watafurahia huduma ya Facebook, Twitter na Wikipedia bure kupitia simu hii,” alisema, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, na kuongeza kuwa simu hizi zinawafaa vijana kutokana na unafuu wake.
Simu hiyo ya Nokia 111 pamoja na huduma nyingine, pia ina kadi ya kumbukumbu yenye uwezo wa GB 32 na kamera.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Nokia nchini, Samson Majwala, amesema wateja wanaweza kupakua programu na michezo mbalimbali kama Fifa 12, Tertis na Need for Speed.
“Simu ya Nokia 111 ina vitu vingi vizuri na rahisi kutumia, itawavutia watumiaji wengi kuzinunua,” alisema Majwala na kuongeza kuwa “Pia ni nzuri kwa watumiaji na zinavutia. Tunaamini kuwa wateja wetu watazifurahia zaidi,”
Kutakuwa na sehemu mbalimbali za mauzo nchi nzima na kuwafika wateja wengi zaidi.
“Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuwaletea huduma nyingi na nzuri ili kukidhi mahitaji yao na kujenga mahusiano mazuri zaidi” alisema Meza.
Post a Comment