ABG NORTH MARA YAGAWA MADAWATI 1,000 KWA SHULE ZA TARIME.
Pichani
Juu na Chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi zilizopo
wilayani Tarime mkoa wa Mara wakifurahia msaada wa madawati zaidi ya
1,000 kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African
Barrick Gold (ABG).
Wanafunzi
wa shule za msingi za serikali za wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara,
wakikaa sakafuni kabla ya kupata msaada wa madawati zaidi ya elfu moja
kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick
Gold (ABG).
Msaada
wa pikipiki tatu maarufu kama Bajaj ambazo mgodi wa North Mara
unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) ulitoa kwa baadhi
ya wananchi wa jamii zinazoishi karibu na mgodi huo uliopo wilaya ya
Tarime mkoa wa Mara.
TARIME
Mgodi
wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick
Gold (ABG) umetoa msaada wa madawati zaidi ya 1,000 kwa shule za msingi
zilizopo wilayani Tarime, mkoa wa Mara.Msaada
huo utakaoenda kwa shule 10 za msingi, utawanufaisha karibu wanafunzi
6,000 ambao kwa sasa wanalazimika kusoma wakiwa wameketi chini kwenye
sakafu ya udongo.
Madawati hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 76.5 yametolewa na kampuni ya ABG kupitia mfuko wake wa maendeleo.
Shule
zitakazofaidika na msaada wa madawati hayo ni Nyangoto, Marare,
Nyamongo,Nyabhigena, Kerende, Genkuru, Bung’eng’e, Nyaisangero,
Nyamwaga, Nyakunguru A na Nyakunguru B.
Shule
hizo zina jumla ya wanafunzi wanaozidi 5,800, huku wanafunzi wengi
wakiwa wanakaa sakafuni kutokana na kukumbwa na upungufu mkubwa wa
madawati.
Akipokea
msaada huo juzi, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele, aliishukuru
kampuni ya ABG na mgodi wake wa North Mara kwa madawati hayo.
Henjewele
alisema kuwa madawati hayo yatasaidia kuondoa kero ya muda mrefu ya
shule hizo ya wanafunzi kukaa sakafuni na hivyo kusoma katika mazingira
magumu.
“Hili
ni tukio la kihistoria ambalo linaonesha jinsi mgodi na watu wanaoishi
eneo hili walivyokuwa na mahusiano mazuri,” alisema.
Walimu pamoja na wanafunzi wa shule za Tarime walifurahia msaada huo na kusema kuwa utasaidia kuboresha mazingira ya elimu.“Tunafuraha
kubwa kukabidhi zaidi ya madawati 1,050 kwa shule zinazozunguka mgodi
wa North Mara na hii inadhihirisha jinsi ambavyo jamii zinavyopata
manufaa kutoka kwenye mgodi wetu,” alisema Meneja Mkuu wa Mgodi wa North
Mara, Gary Chapman.
Msaada
huo wa madawati ulienda sambamba na kuzinduliwa kwa program ya Can
Educate ambayo inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye uwezo ambao
wanatoka kwenye jamii maskini.Mgodi huo pia ulitoa msaada wa pikipiki za Bajaj kwa wanakijiji watatu wenye ulemavu wa viungo.Mgodi
wa North Mara umekuwa ukitoa misaada mingi ya jamii zinazozunguka
mgodi huo kwenye sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu na uwezeshaji
wa kiuchumi.
Uongozi
wa kampuni ya ABG pamoja na mgodi wa North Mara umekuwa ukifanya
jitihafa kubwa kuboresha mahusiano na jamii zinazozunguka mgodi huo.
Post a Comment