Bingwa mara saba wa mashindano ya baiskeli yajulikanao kama Tour De France, Lance Amstrong amepoteza kila kitu yakiwemo mataji saba aliyokuwa ameyashinda pamoja na mikataba, kufungiwa kujihusha na mashindano hayo kwa maisha na makampuni yaliokuwa yanamdhamini mara baada ya kugundulika alikuwa anatumia madawa ya kuongeza nguvu na yaliokatzwa michezoni na idara ya kuzuia utumiaji madawa haramu ya United States Anti-Doping Agency (USADA).
Mwanamichezo huyo anayetokea katika jimbo la Texan nchini Marekani alipatwa na kashfa hiyo mara baada ya idara hiyo kutoa ripoti yake mwishoni mwa mwezi uliopita na kuonyesha Amstrong amekuwa na tabia ya kutumia madawa hayo na hivyo kufungiwa maisha katika kujihusisha na mashindano hayo tena.
Itakumbukwa Amstrong aliibukia mnamo mwaka 1999 mara baada ya kupona katika ugonjwa wa Kansa na kujishindia mataji saba mfufulizo.
alilala tajiri kaamka maskini, Kampuni ya miwani ya Oakley imekuwa kampuni ya hivi karibuni kusitisha mkataba na bingwa huyu wa zamani mara baada ya makampuni mengine ya Nike, Trek ya Anheuser-Busch kufanya hivyo wiki iliyopita. |
Lance Amstrong enzi zake katika kutesa katika mashindano ya baiskeli |
hakuna kama mimi, Lance Amstrong
Post a Comment