Manchster united fightback, Blues lose, Barca scare
Manchester United ilibidi watoke nyuma ili kushinda 3-2 dhidi ya Braga kwenye michezo ya Kalbu bingwa ya Ulaya, Mabingwa Watetezi Chelsea wamefungwa na y Shakhtar wakati Celtic walikuwa bado kiduchu tuu wapate ushindi wa kihihistoria dhidi ya magwiji wa Uhispania timu ya Barcelona katika uwanja wao wa Nou Camp sasa fuatilia mwenyewe kupitia picha..
Timu mabingwa wa Uhispania, Barcelona jana usiku ilibidi wasubiri hadi dakika za mwisho za nyongeza ndio waweze kufanikiwa kupata ushindi mwembamba wa magoli 2-1 dhidi ya mabingwa wa Scotland Celtic.
Kama ilivyokuwa imetabiriwa kabla ya kuanza kwa mpambano huo ya kuwa mabingwa hao wa Scotland wanaweza kufanya maajabu ndani ya uwanja wa Nou Camp na ndivyo ilivyotokea kukaribia kuondoka na point moja sasa wadau wa soka watakuwa na maswali kibao huu ndio mwisho wa Barcelona????

kipa wa Celtic, Fraser Forster akiwa amejifunika uso kwa uchungu wa kupoteza mchezo wa jana katika dakika za lala salama.

Lionel Messi akiwa na shujaa wa mchezo wa jana Jordi Alba.
Man Utd 3 Braga 2.Fergie Alalamikia sehemu ya ulinzi
Mara nane wameruhusu timu pinzani kuanza kufunga na mara sita waliweza kuzawisha na kupata ushindi lakini hiyo haikumzuia Sir, ALex Ferguson ameendelea kulia na sehemu ya ulinzi ya timu yake mara baada ya timu hiyo kuruhusu mabao mawili , aliendelea kusema sijui nini kinatokea kwa sasa ila cha msingi tushukuru safu ya ushambuliaji inajitahidi kuficha yote yanatokea katika safu ya ulinzi.Feruson akusita kumsifia Javier Hernandez kwa magoli ya mawili na kusema kwa kweli kijana anafanya vizuri sana mazoezini na hata kwenye michezo sasa sijui itakuaje maanake yuko yeye, Robin Van Persie, Wayne Rooney na Danny Welbek.

WAyne Rooney akimpongeza Chicharito baada ya kuisaidia Manchester United kutoka kifua mbele 3-2 dhidi ya Braga jana usiku.


Javier Hernandez akishangilia goli lake la pili na la ushindi jana dhidi ya Braga.

De Gear akiruka bila mafanikio kuzuia kichwa cha Alan na kuipatia timu yake goli la kuongoza

Akiruka kama mkizi hapa akifunga goli la ushindi
Shakhtar Donetsk 2 Chelsea 1

kama vile Ramirez amuamaini kile Alex Teixeira anachokiongea au kukimaanisha ila mwisho wa mchezo ilibidi akubaliane na kilichokuwa kinamaanishwa.

Shaktar Donetsk wakishangilia kwa furaha ushindi wao wa jana 2-1 dhidi ya Mabingwa watetezi wa kombe hilo Chelsea ya Uingereza.

Inavyoelekea hii beji ya Unite Against Racism ilikuwa ni mzigo kwa Nahodha wa Chelsea, John Terry

Mfungaji wa goli la ushindi, Alex akishangilia kwa kunyoosha mikono juu mbele ya Ramirez

kipa Cech akiwa katika moja ya dhawama zilizoelekezwa langoni mwake jana

Huyu ndi Dinho wao ajulikanae kama Fernandinho akiwazidi ujanja David Luiz na Petr Cech
Vucinic saves Juve blushes
![]() |
Mchezaji wa Nordsjaelland Mikkel Beckmann akiiaptia timu yake goli kupitia mkwaju wa free-kiki dhidi ya Juventus. |
Muller akiipatia Bayern Munich ushindi ugenini dhidi ya Lile.

Thomas Muller akiifungia Bayern goli kwa njia ya tuta dhidi ya Lile na kuisaida kuibuka na ushindi wa 1-0
Soldado wazamisha BATE Borisov
Roberto Soldado awa mwiba mkali kwa mabingwa wa Belarusia, BATE Borisov kwa kupachicha mabao matatu maarufu kama Hat-Trick na kuwanyamzisha mashabiki elfu kumi na saba elfu 17,000 waliokuwa wamehudhuaria mpano huo.

Robert Soldado akifunga mojawapo ya magoli yake yaliyowazamisha BATE katika ushindi wa 3-0 katika uwanja wa Dynamo, Minsk.
Post a Comment