Picture

Msanii Kalapina wa kikosi cha mizinga ameamua kuweka wazi kwa nini anaona serikali inafanya masihara kwenye sekta ya Afya.

Namkariri akisema “juzi nilikua Muhimbili nasumbuliwa na vidonda vya tumbo kuna kipimo kinaitwa OGD cha kupima mfumo mzima wa chakula, kile kipimo Muhimbili hakipo na wakati kipo kinafanya kazi gharama ilikua laki moja, ni pesa nyingi sana kwa mlalahoi kumudu”

“hawa madaktari wanapogoma wanahaki ya kugoma kutokana na hakuna vitendeakazi watanzania wanakufa, sekta ya afya ni sekta muhimu sana wabongo wanapiga kelele tu serikali inakusanya mapato mengi wawekezaji wamewekeza kwenye migodi, kwenye kila sekta lakini tunashindwa kuelewa serikali inashindwa nini kuboresha huduma za afya, inakusanya kodi hizi pesa zinakwenda wapi? huduma ya afya inabidi itolewe bure”

kwenye line nyingine kuhusu Dr Ulimboka, Kala amesema ni mpiganaji, hamshauri kabisa aondoke nchi hii kwa sababu mchango wake na taaluma yake inahitajika, haya madaktari walio nje ya Tanzania warudi nyumbani.

---
Habari via MillardAyo.com












































































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.