Wanafunzi 80 wa shule za sekondari za Ilala wamezawadiwa kwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha tatu na tano.
Tuzo hizo zilitolewa Dar es Salaama na Wakuu wa Shule Tanzania (TAHOSSA) katika hafla iliyofanyika kwenye sekondari ya Tambaza.
Akitoa
taarifa ya uendeshaji wa mitihani Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani
Ilala, Hussein Zuberi alisema kuwa umoja huo lengo lake kuunga jitihada
za serikali katika kukuza taaluma katika shule zote za serikali hapa
nchini.
Zuberi alisema kuwa mitihani hiyo huendeshwa katika ngazi
ya Kanda na mikoa ,kama ilivyo katika mkoa huo wa Ilala na hiyo ni mara
ya kwanza kwa kamati hiyo kuendesha mitihani kwenye ngazi ya
mkoa, "Kamati ya mitihani Mkoa Ilala TAHOSSA huendesha mitihani uendesha
mitihani ya kumaliza mwaka wa masomo kwa kidato cha tatu na kidato cha
tano kila mwaka na washindi upewa zawadi, kidato cha tatu wanafunzi 41,
kidato cha tano wanafunzi 39," alisema Zuberi.
Madhumuni ya
mitihani hiyo kuwajengea wanafunzi hali ya ushindani,kuwasaidia walimu
kupata uzoefu katika utungaji,kuhariri, kusahihisha mitihani,kusaidia
walimu kujua uwezo wa wanafunzi wao.
Kwa upande wake Mbunge wa
Tarime, Nyambari Chacha alisema kuwa wamebaini kitu kizuri kwa wanafunzi
wa shule hizo ili waweze kujihamini huko mbele, na kuwataka wazazi
kushirikiana na kamati za shule katika kufatilia maendeleo ya watoto
wao.
Chacha aliwapongeza mpango huo na kusema kuwa mtaala wa
elimu uwe unabadilika kila wakati kutokana na mabadiriko tuliyonayo, pia
kabla kubadirisha kwa mtala huo tuwandae walimuwatakaofundisha.
Aliutaka umoja huo wa TAHOSSA kusimamia vizuri shule za kata hili ziweze kutoa wanafunzi bora watakaojenga Tanzania ya baadae.
---
Habari imeandikwa na Heri Shaaban via gazeti la Majira
Post a Comment