Baada ya Serikali kutoa kauli kuhusu mtihani wa Taifa wa kidato cha nne
mwaka jana, Mbunge James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ametaka Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, awajibike na ikiwezekana
akamatwe na kushitakiwa.
Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi |
Kauli hiyo aliitoa jana kwa waandishi wa
habari akisema kuvurugika kwa utaratibu kutokana na kuanzisha utaratibu
mpya wa usahihishaji na kutoa alama bila kushirikisha wadau, unamgusa
Waziri ambaye ndiye mwenye dhamana.
Alisema watu wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) hawawezi kufanya uamuzi bila kujulikana na watu wengine wa juu akiwamo Waziri na kusababisha wanafunzi wengi kufeli mitihani ya kidato cha nne mwaka jana.
Aidha, Mbatia alisema kwa mantiki na falsafa ya utendaji haiwezekani utaratibu huo ukakosa baraka za Waziri wa Elimu.
“Si kujiuzulu tu kuna watu wanatakiwa wakamatwe na kushitakiwa kwa kosa hili, kwa kuwa limefanyika kwa makusudi…limetengenezwa, halikutokea kwa bahati mbaya,” alisema.
Mbatia ambaye alifuatana na Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema Dk Kawambwa alitakiwa kwa ripoti ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, asionekane hadharani kwa sababu ni aibu kwake.
Aidha, alisema Tume
iliyoundwa na Waziri Mkuu kuchunguza kufeli kwa wanafunzi hao, imebeba
asilimia 75 ya maudhui ya hoja yake aliyoiwasilisha bungeni kuhusu
udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini mwaka jana.
Aidha, alisema ni vema wanasiasa na watu wengine wakakubaliana na ukweli wa kusikiliza hoja na kuacha ushabiki wa kisiasa.
“Hatuwezi
kusubiri Rais na Waziri Mkuu kuwa viranja wa kuhakiki mawazo
yanayotolewa na wananchi. Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote kuleta
mabadiliko . La msingi ni taarifa na si mtoa taarifa,” alisema na
kuongeza:
“Hata mwendawazimu ana haki ya kusikilizwa. Kama hoja yangu
ingelipokewa na Bunge, hatua kadhaa nilizopendekeza zingekuwa
zimetekelezwa na Taifa lingejiepusha na aibu hii.”
Aidha, Mbatia
ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema ripoti hiyo
inaliamsha Bunge kutoka usingizi wa kutumia itikadi za vyama kufanya
uamuzi.
Alisema aliyesoma au kusikiliza hoja yake,
amethibitishiwa na ripoti ya Tume ya Waziri Mkuu kwamba misimamo ya
kiitikadi bungeni ni adui wa maendeleo ya Taifa.
Post a Comment