Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
Kanisa lililojengwa kwa ajili ya
kumbukumbu ya makanisa ya kale yaliyojengwa enzi za ukoloni yapata miaka 100 ambapo
watemi wa kabila la wasukuma walikuwa wakiabudu .
Ni kama kigoda vile umbo la jengo
hili ambako ndiko kulitumika kuhifadhi ngoma za asili zilizotumiwa na
wanasanaa wa kabila la Wasukuma katika koo mbalimbali ngoma hizi
zimehifadhiwa yapata miaka 100 sasa .
Mdau Madata Ndelule Charles mhifadhi mwandamizi wa
makumbusho hayo akionyesha mfano wa nyumba ambayo watemi
waliishi.
Bagika na Bagalu ni ngoma za pande
mbili ndani ya kabila la Wasukuma ambapo Bagika walikuwa wakicheza ngoma
inayoshirikisha nyoka na Bagalu walikuwa wakicheza ngoma
inayoshirikisha zana kama majembe ya mkono, zana za kale za kivita.Kikundi cha sanaa cha Bujora group
Zana na nyenzo za enzi za kale zilizotumika katika usagaji nafaka ili kupatikana unga.
Hatua kwa hatua usagaji nafaka kwa kutumia zana na kale huku nyimbo asili zikitawala .Habari na picha kwa msaada wa blogu ya http://netnewstz.blogspot.com
Wabeja Sana Mw'ana Makangale.
ReplyDelete