Timu ya Bayern Munich kutoka Ujerumani jana usiku ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Klabu bingwa ya Ulaya. Walikuwa ni wachezaji Arjen Robben na Mario Mandzukic waliofanikiwa kuifungia timu hiyo bao moja kila mmoja na kufanikiwa kuipatia timu yao ya Bayern ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya mahasimu wao wakuu wa soka la ujerumani timu ya Borrusia Dortmund.
Itakumbukwa katika fainali zilizopita zilizofanyika katika uwanja wa Allianze Arena wa Bayern Munich timu hiyo ilishindwa kutwaa kombe hilo mbele ya timu ya Chelsea ya mjini London na Arjen kukosa mkwaju wa penati katika muda wa nyongeza na pia katika fainali za mwaka 2010 dhidi ya Inter Milan mchezaji huo pia alikuwepo na katika mashuti yake 24 aliyoyapiga sawa na jana hayakufanikiwa kupata bao mpaka alipofanikiwa kupiga shuti lake la 25 ambalo ndilo liliflofanikiwa kuondoa mzimu wa kukosa kufunga katika fainali zote mbili alizofanikiwa kuichezea timu hiyo na kuipatia timu yake goli la ushindi.

Nyota wa Mchezo wa jana , Arjen akiwa ameshikilia kombel Ulaya kwa furaha pasipo kifani.

Wafungaji wa mabao yaliyoipatia timu ya Bayern Ubingwa jana, Arjen Robben na Mario Mandzukic wakishangilia kwa pamoja.


Mchezaji wa Borussia Dortmund, Blaszczykowski akisikitia mara baada ya kukosa kufunga.


Mashabiki wa Bayern Munich wakilipuka kwa furaha kwa kutimu yao kushinda kombe la klabu bingwa ya Ulaya.

Post a Comment