Mchezaji  nyota anayechupikia katika soka la dunia na kutajwa kama mmoja wa nyota wa baadae wa soka  kwa Brazili katika kufuata nyayo za mastaa wengine kama vile Pele, Ronaldo De Lima, Bebeto, Romario na wengine wengi , Neymar anayeichezea wa timu ya Santos ameamua kuichagua timu ya Barcelona.

 Itakumbukwa ya kwamba timu hiyo ya Brazil kufika mwishoni mwa wiki hii ilikuwa imekubali kupokea ofa kutoka kwenye klabu mbili maarufu na kubwa za uhispania, timu za Barcelona na Real Madrid na ikawa imebakia kwa mchezaji huo kusema wapi anapotaka kuelekea.

Na kulingana na ujumbe aliooandika mchezaji huo kupitia mtandao wa kijamii unaojulikana kama Instagram, mchezaji huyo ametabanaisha ya kuwa mara baada ya kupata mawazo kutoka kwa marafiki zake na familia yake ameamua kujiunga na Barcelona na siku ya Jumatatu o ujumbe wa Barcelona unatarajiwa kuelekea mjini Sao Paolo kwenda kumalizia kumsanisha mchezaji kwa tarkibani ada ya kiasi cha paundi za kiingereza zipatazo milioni 20.

Mchezaji huyo ambaye ni mmoja wa nyota wanaotajwa kutoka barani America ya kusini kwa sasa hadi kufikia kuhama kwake alifanikiwa kuifungia timu yake ya Santos jumla ya mabao 138 katika michezo 229 aliyoichezea timu hiyo kuanzia mwaka 209.




Mchezaji Neyamar akiwa na timu yake ya Taifa ya Brazil



Neymar

Mchezaji wa Santos na timu ya taifa ya Brazil, Neymar ambaye amekubali kuhamia kwa mabingwa wa sasa wa Uhispania, timu ya Barcelona yenye makao yake makuu ndani ya uwanja wa Nou Camp.












































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.