Jana usiku mchezaji toka Uingereza aliweka rekodi kwa kuwa muuingereza wa kwanza kushinda mataji manne katika nchi nne tofauti mara baada ya timu yake ya sasa Paris Saint Germany kushinda kwa goli moja kwa bila 1-0 dhidi ya timu ya Lyon katika ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1
Itakumbukwa mchezaji huo amefanya hivyo akiwa na timu za Manchester United, Real Madrid ya uhispania na LA Galaxy ya marekani.
Goli lililohihakikishia St German kunyakua kombe hilo lilifungwa katika dakika ya 53 na mchezaji Jeremy Mendez. Hata hivyo timu hiyo itabidi kusubiria hatima yao kutoka kamati ya nidhamu ya ligi hiyo dhidi ya kupokonywa pointi kutokana na madai ya mkurugenzi wao Ufundi, Leornado kumsumbua mwamuzi.
Post a Comment