Na Mwandishi
Wetu, Mbeya.
MKUU wa Mkoa wa
Mbeya, Abbas Kandoro ameipongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kutokana na bia
ya Safari Lager kutwaa Tuzo ya Bia Bora Afrika.
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akizungumza
na wananchi wa Mji wa Mbeya wakati upokeaji Tuzo za Bia ya Safari Lager mkoani
kwake jana ikiwa ni ziara maalum ya Tuzo hizo kusherehekea pamoja na Watanzania
Ushindi wa Bia hiyo ya Kitanzania barani Afrika.Ziara ya Tuzo za Bia ya Safari
Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilikuwa Mkoani Mbeya. Kushot ni Meneja wa Bia
ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (Picha
na Mpigapicha wetu). |
Kandoro
alimwaga sifa hizo wakati akipokea kombe la ushindi huo ambalo lilioneshwa
mahususi kwa wakazi wa Mbeya, katika sherehe zilizofanyika kwenye Viwanja vya
Kabwe vilivyopo Mwanjelwa mjini hapa jana.
|
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
akimkabidhi rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (kulia)
Tuzo za Bia ya Safari Lager ilizoshinda katika mashindano ya Bia Afrika
yaliyofanyika nchini Ghana. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa ziara
maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo ilizoshinda Bia yake ya
Safari Lager ambapo jana walikuwa Mkoani Mbeya. (Picha na Mpigapicha wetu). |
Alisema ni
faraja kubwa kwa Watanzania kutokana na bia ya Safari Lager kutwaa tuzo hiyo na
kufanikiwa kuzishinda bia zote barani Afrika kwa ubora.
|
Wakazi wa Mji wa Mmbeya wakiwa wamefurika kwa
wingi wakishuhudia Burudani na Tuzo mbili zilizotwaliwa na Bia ya Safari Lager
inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika mashindano ya Bia Afrika
yaliyofanyika Nchini Ghana. (Picha na
Mpigapicha wetu |
“Tunashukuru
tumeletewa kuliona kombe mlilolipata kutokana na ubora wa bia yenu, hii ni
furaha kwa Watanzania na naamini ushindi huu utachochea watu kupenda bidhaa
zao.
“Kufanikiwa
kutwaa Tuzo ya Bia Bora Afrika si kitu kidogo, ni faraja kwetu sote na sasa
tunaweza kujivunia kile kilicho chetu,” alisema Kandoro.
Sherehe hiyo ya
kulionyesha kombe kwa wakazi wa Mbeya kuliambatana na burudani za kila aina,
ambazo zilitolewa na vikundi kadhaa vya muziki.
Akizungumzia
ushindi huo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema ni wa
kujivunia zaidi na wao watahakikisha wanaendelea kuzalisha bidhaa bora zaidi.
Safari Lager
imefanikiwa kushinda tuzo hiyo, kutokana na shindano lililofanyika Accra, Ghana
na kushirikisha bia zote zinazozalishwa barani Afrika.
Post a Comment