Mapenzi,
kama ilivyo kwa vitu vyote hapa ulimwenguni, hayawezi kuwepo bila
kujumuishwa na fizikia na kemia yake! Bila kemia hakuna mapenzi ya
kudumu. Tamaa ya ngono kimsingi huanza pindi unapokutana na mtu. Tamaa
hiyo huweza kukua na kuwa kitu kingine kadiri muda unavyokwenda lakini
chanzo kinakuwepo toka siku ya kwanza mlipokutana. Kemikali
inayosababisha tamaa ya ngono na hata kuikuza tamaa hiyo ni 'phenyl
ethylamine' ('fino itholamine') au PEA ambayo ni kemikali ya mapenzi
ndani ya ubongo.

Husisimua watu na huongeza nguvu za kimwili (fizikia) na kihisia (kemia). Tamaa husababisha mtu azalishe PEA nyingi zaidi, kitu kinachosababisha kujisikia kizunguzungu (cha hisia za kimapenzi) na dalili zingine kama magoti kutetemeka, jasho kutoka viganjani na kutokutulia. Kemikali hii inapozalishwa kwa kiwango kikubwa, hutuma alamu ('signals') kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye viungo vingine vya mwili na kutumika kama 'dopamine' au 'amphetamine' ambazo ni kemikali za ulevi ndani ya ubongo. Iwapo unajiuliza kwa nini wewe au mtu mwingine unavutiwa na mtu ambaye hamwendani kimapenzi, inaweza kuwa ni kwa sababu una kiwango kikubwa cha kemikali hizo kuliko mwenzako, kitu ambacho huzidi uwezo wa kutumia kichwa na kutoa maamuzi bora kulingana na akili ya kuzaliwa.

Habari na Enock Maregesi
Chemistry zikilingana watu wataweza kupendabna milele
ReplyDeletemapenzi ni madawa,kwani hulevya ka madawa ya kulevya.Very informative.
ReplyDelete