Maonyesho ya vyuo vikuu ya 8 yanayoandaliwa na Tume ya kusimami vyuo vikuu nchini TCU ( Tanzania Comission for Universities) yamezindulia leo rasmi jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee na Makamu wa Raisi, Dr. Gharib Billal. Maonyesho hayo yatakayokuwa dumu kwa siku tatu kuanzia tarehe 21st May 2013 hadi 24th May 2013.
Maonyesho hayo yanaoshirikisha vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi yalio na maudhui ya kujenga jamii endelevu, yenye kuwajibika pupitia elimu ya juu ya sayansi na teknolojia kama ujumbe mkuu wa maonyesho hayo kwa mwaka huu.
Mgeni Rasmi katika unfunguzi wa maonyeshoa hayo makamu wa Raisi , Dr Gharib Billal akitoka kutoa hotuba ya ufunguzi na kuelekea yalipo mabanda ya maonyesho hayo kwa ajili ya yeye mwenyewe kushuhudia kile alichokizindua.
Umati wa wakazi wa Dar es Salaam wakiwa wanatembelea mabanda ya maonyesho ya Vyuo Vikuuu yaliyoandaliwa na TCU
Mgeni Rasmi, Makamu wa Rais, Dr. Gharib Bilali akipata maelekezo toka kwa mmoja wa wahusika wa mabanda hayo ya maonyesho |
Msafara wa Makamu wa Raisi ukiwa makini kupata maelekezo toka kwa washiriki wa maonyesho hayo
Banda la Open University of Tanzania (OUT) |
umati wa wakazii wa mjini Dar es Salaam ukiwa ndni ya mabanda hayo kupata maelekezo mbalimbali kuhus na taarifa za masomo |
Mabanda ya University of Dar es Salaam na vyuo na vitengo vilivyo chini yake kama DUCE, UCC na vinginevyo katika picha
Moja ya kivutio kikubwa katika maonyesho hayo ni moja ya magari ambayo yameweza kutengenezwa nammoja wa wanafunzi wa vyuo hivyo kutoka korea yanayotumia nguvu ya umeme katika kusafiri, kulingana na maelezo ni kuwa gari hilo linaweza kuchajiwa kwa muda wa masaa 5 na kutembea kwa kilimota elfu moja
pia linaweza kujicharge pasipo kuwekwa kwenye umeme kwa kutumia mfumo wa wireless endapo litakuwa limeegeshwa maeneo yanaoweza kutengeza nguvu ya umeme.
Mfumo wa Wireless Chager ukiwa pichani katika kuelekeza namna gari hilo linavyoweza kujicharge.
Mgeni RAsmi akiwa anatembelea mabanda ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi, Makamu wa Raisi, Dr. Gharib Billal akibadilishana jambo na mmmoja wa waliokuwa nae kwenye msafara.
Post a Comment