Mchezaji David Beckham (38) ambaye majuzi alifanikiwa kuandika rekodi kama mchezaji wa kwanzaa toka nchini Uingereza kufanikiwa kutwaa makombe ya michuano ya Ligi nne tofauti duniani hatimaye ametangaza rasmi ya kuwa mara baaday ya mchezo wa mwisho wa ligi mnamo tarehe 26 mwezi huu ndio utakuwa mchezo wake wa mwisho katika soka. Japokuwa mchezaji huyo alikuwa ameahidiwa nafasi nyingine tena ya kuon geza mkataba wake klabuni hapo amesema amefikia uamuzi huo akiwa anataka kuachana na soka akiwa bado na kiwango cha juu.
Itakumbukwa ya kwamba DAvid Beckham ambaye alianzia maisha yake ya soka tangia akiwa na umri wa miakaa 11 akiwa na timu ya Manchester United amepata kuzichezea timu tano tofauti duniani ikiwamo ni pamoja na Manchester United, Real MAdrid ya Spain, LA Galaxy ya Marekani, Ac Milani ya Italy na mwisho kabisa kumalizia soka lake na timu mabingwa wa sasa wa Ligue 1 ya Ufaransa , timu ya Paris St. Germany, Beckam ameichezea Manchester mechi 394 na kufunga jumla ya magoli 85 na pia aliichezea timu yake ya taifa mechi 115 na kuafanikiwa kuifungia magoli 17 tangia alipoanza kuichezea mnamo mwaka 1996.
Itakumbukwa pia ya kwamba kocha aliyemuwezesha David Beckham kufikia mafanikio yake yoye hayo, Sir Alex Ferguson pia ametangaza kustaafu ifikapo mwishoni mwa msimu huu.
Beackham akiwa ndni ya jezi ya timu yake ya sasa, Paris St Germany
Marafiki wa kweli, Beckham na Gary Neville wakiwa katika timu ya Taifa.
All photos by www.thesun.co.uk
Post a Comment