OMBI KWA MHE RAIS JAKAYA KIKWETE
OKOA ARDHI YETU NA MAISHA YETU

1.    Utangulizi

Mhe Rais, Tuliwatuma viongozi wetu wa kisiasa na wawakilishi wa wananchi kwenda Dodoma kuonana na Mhe Waziri Mkuu, viongozi wa Chama na viongozi wengine. Taarifa waliyotuletea ilitutaarifu kuwa sasa tatizo la ardhi yetu litapelekwa Kwa Mheshimiwa Rais kwa mashauriano zaidi. Mpaka sasa hatujapata jibu lolote. Kutokana na kukosa jibu la jambo hili sisi Viongozi wa Kimila (Malaigwanani) tumeona ni vyema tukaonana na Mhe Raisi ili kujua hatma ya jambo hili. Lakini kwa kuwa imekuwa vigumu kupata nafasi ya kuonana na Mhe Rais ana kwa ana imetupasa kumfikishia ujumbe kupitia vyombo vya habari.

2.    Hoja yetu ya Leo
Mhe Rais, Mpaka sasa, imepita takriban mwezi mzima kutoka mkutano wa viongozi wetu wa kisiasa na Waziri Mkuu na viongozi wa Chama na bado taarifa yeyote haijapatikana ya suluhu ya tatizo letu la ardhi. Hali ya wasiwasi inaendelea kutawala na shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi hazifanyiki kwa sasa huko Loliondo. Kwa kuwa sisi ndio wenye sauti ya mwisho kwenye jamii, tumeonelea ni vyema tuje kufikisha suala kwa Mhe Rais  baada ya makundi mengine kusemea bila mafanikio. Ndio sababu tunatoa ombi hili kwa  Mhe Rais.

Mhe Rais, Sisi Mailagwanani wa Mila wa KiMaasai kutoka Loliondo wilaya ya Ngorongoro tunakuomba na kukusihi kuwa Serikali isichukuwe ardhi yetu kwani kufanya hivyo itaathiri mfumo wa maisha yetu ya kifugaji kiuchumi na kijamii. Aidha itatukumbusha machungu ya kumbukumbu ya kuhamishwa kwetu kutoka Serengeti na Serikali kwa ajili ya uhifadhi kama ilivyofanya mwaka 1959. Na kwakuwa sisi ndio wenye jukumu la kusimamia utulivu na amani kwenye jamii tumeona ni vyema tukamuomba Raisi alipatie ufumbuzi suala hili mapema ili kuiacha Ngorongoro katika hali ya amani.Kwani hadi sasa tumesha watuliza wanachi wenye hasira na mpango huu wa kumega ardhi yao hadi tumechoka.

Mhe Rais, Kwa miaka mingi,  sisi wafugaji wa jamii ya Kimasai tumekuwa mstari wa mbele kutunza mazingira ya mbuga ya Serengeti na viunga vyake, na tutaendelea kufanya hivyo kwa kushirikiana na serikali. Hili ndio ombi letu kwako kwa niaba ya wananchi 71,000 ambao watakaoathirika na mpango huu na ambao wamekuwa wasikivu kwa Serikali  kwa muda  huu wote.

Mhe Rais, Kwa kuwa serikali inatambua umiliki wa ardhi ya vijiji vyetu kisheria na iwapo Serikali itaamua kuchukua ardhi yetu Serikali itakuwa imekiuka haki za msingi pamoja  na   sheria za nchi. Na kwa mantiki hiyo,  haitakuwa na maana tena kwa vijiji vya Loliondo pamoja na vijiji vingine nchini  kumilikishwa ardhi kisheria.

Mhe Rais, sisi Malaigwanani tumesikitishwa, kusononeshwa na tumedhalilishwa na kauli za mawaziri mbalimbali hususan wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutuita Wakenya kila wakati wakitaka kuchukua ardhi yetu. Lakini pia, tunalaani kauli za vitisho vinavyotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali kwa viongozi na watetezi wa ardhi ya wafugaji Loliondo. Kwa kuwa mawaziri wamekuwa wakituita wakenya  tunakusihi Mhe Rais  uwatake mawaziri wakanushe kauli zao kwani wanaoishi Loliondo si Wakenya na  kauli hizo zinapotosha uhalisia wa tatizo lenyewe. Aidha adhima yetu ya kutaka kuonana nawe Mhe. Rais bado ipo pale pale , hivyo tunakusihi utufungulie milango kwa wakati muafaka.




 


Sisi Malaigwanani wa Jamii ya Wamasai kutoka wilaya ya Ngorongoro

S/N
JINA KAMILI
CHEO
ENEO
SAHIHI
1
Joseph Tiripai
Mwenyekiti
Pinyiny

2
Laanoi Munge
Katibu
Arash

3
Justin Nokoren
Aligwanani
Piyaya

4
Kashanga Pusalet
Aligwanani
Olorien

5
Lekakui Kanduli
Aligwanani
Maaloni

6
Mshao Naingisa
Aligwanani
Ololosokwan

7
Luka Olotilimu
Aligwanani
Malambo

8
Ikayo Mbalala
Aligwanani
Oloipiri

9
Konini Ng’atuny
Aligwanani
Arash

10
Joshua Ngoitoi
Aligwanani
Soitsambu

11
Kaiki Konorei
Aligwanani
Olorien

12
John Kulinja
Aligwanani
Malambo

13
Mathew Timan
Mzee Mashuhuri
Ololosokwan

Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.