Imetangawzwa leo na katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) Bwana Gianni Infantino, ya kuwa kuanzia msimu wa2015/2016 timu itakayokuwa bingwa wa Europa League atakuwa anaingia moja kwa moja katika mashindano ya Champions League.
Mabadilikio hayo yatakuwa kama chachu ya kuongeza ushindani katika ligi ya Europa na kufanya klabu kushindana wakiwa wanajua ya kwamba hata kama wakishindwa kupata nafasi za kuingia kupitia ngazi za mashindano ya ligi ya nyumbani kuna uwezekano huo kupitia kuwa Bingwa wa Europa.
Kwa mantiki hiyo kama sheria hiyo ingeanza msimu unaokuja wa 2013/2014 timu ya chelsea ingefaidika na mabadiliko hayo kama ingekuwa imeshindwa kupata nafasi nne za juu katika Ligi kuu ya Uingereza.
Mabingwa wa sasa wa Europa Ligi, Chelsea |
Post a Comment