Tanzania Human Rights Defenders Coalition [THRD-Coalition]
P. O.
Box 105926 Dar es Salaam, TANZANIA
Telephone: +255-22-2773038/48, Fax: +255-22-2773037, Mob: +255 783 172394
E-mail: defenderscoalition@rocketmail.com, web www.thrdcoalition.com
TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU
(THRD-COALITION) KUPINGA KUKAMATWA KWA MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WILAYA YA
BAHI
BB DOMINIC HAULE NA WENZAKE SITA
Mtandao wetu umezipokea kwa
majonzi habari za kukamatwa kwa mwanachama wake na Mtetezi wa Haki za Binadamu
BB Dominic Haule na wenzake sita. Waliokamatwa ni Mpumba Mwaruko, Juma Kamunya,
Charles Munyakongo, Ayubu Mukosi, Matereka Ndoru, na Champunga Mburi Mutinya.
Taarifa tulizozipokea kutoka
eneo hilo zinasema Bw Haule na wenzake wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa
kutimiza majukumu yao kama raia wema wanaotaka kuona kwamba utawala wa sheria
na haki unazingatiwa. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu hivyo vya habari watetezi hao
wakiwamo waandishi wa habari walikuwa wanafuatilia mambo yaliyokuwa
yanalalamikiwa na wananchi ambayo ni pamoja na kutozwa michango mikubwa bila
kuona manufaa ya kile wanachochangia.
Baadhi ya maeneo yaliyokuwa
yanaathiriwa na ukiukwaji huo wa haki za binadamu ni Kijiji cha Chali Isanga,
Wilayani Bahi ambalo ni eneo lililo chini ya uangalizi wa Utetezi wa Haki za
Binadamu wa Bw BB Dominic Haule. Vyanzo vyetu vinaeleza kwamba ukiukwaji huo ni
pamoja na watu kutozwa hadi shilingi la saba kwa mtu mmoja kwa ajili ya
michango hiyo kulingana na idadi ya mifugo aliyonayo.
Pia kulikuwa na fedha
zilizokuwa zimechangwa kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule pamoja na Wadi ya
Kujifungulia akina mama kijijini hapo bila kukamilika. Katika ujenzi huo jengo hilo
liliezekwa kwa mabati ya zamani na kupakwa rangi huku ikielezwa kuwa ni mapya
jambo ambalo wananchi walilipinga.
Pia katika hatua hiyo
ilibainika kwamba baadhi ya vifaa vya ujenzi vimeuzwa na baadhi ya viongozi wa
kijiji kwa watu wasiohusika na katika kutaka kufukia habari hiyo wakaamua
kuzuia waandishi wasijue chochote
Mnamo tarehe 24 Aprili Bw BB
Dominic alitafuta mwandishi wa habari na kwenda naye kijijini na wakati wakiwa
kijijini hapo katika kazi ya uchunguzi walikutana na wananchi waliowapa
ushirikiano na kuwaonyesha baadhi ya vifaa vya ujenzi wa zahanati vilivyoibwa
na viongozi na kuuzwa kwa watu wasiohusika.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Board
of Directors:
Dr.
Helen Kijo Bisimba, Kharous Mpatani, Martina Kabisama, Tike Mwaipabipile,
Joseph Parsambei,
Saed
Kubenea, Hamisa Mmanga and Ernest Kimaya.
Wakati wakihojiana na
wanavijiji hao, alifika Afisa Mtendaji wa Kata (WEO), na kuanza kuhoji uhalali
wa mwandishi wa habari kufika kijijini hapo ambapo alimtaka aonyeshe
kitambulisho chake cha kazi.
Huku akiwa ni mwenye hasira
kali na kwa woga wa kuumbuliwa katika vyombo vya habari alikitupa chini
kitambulisho hicho na akakipiga teke kisha kumpiga ngumi mwandishi huo wa REDIO
KIFIMBO na kusababisha kupoteza baadhi ya vifaa vyake vya kazi.
Kitendo cha kupigwa kwa
mwanahabari Maliki Selemani kiliwakera wananchi na hasa baada ya kuona kwamba
waliyemtegemea kulinda amani ndiye anakiuka haki za binadamu na kumpiga
mwandishi asiye na hatia. Na hapo ikatokea purukushani kati ya wanakijiji na
mtendaji huyo. Baada ya tukio hilo
mtendaji huyo wa Kata ya Chali Isanga alitoweka katika mazingira ya kutatanisha
na siku ya pili yake alifika akiwa na askari na kuanza kuwakamata baadhi ya
wananchi.
Inadaiwa kukamatwa huko
kunafuatia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwasa, hadi sasa Mtetezi
BB Dominic na wananchi wengine sita wamekamatwa, kufunguliwa shitaka la
uchochezi na kusababisha vurugu kijijini. Baada ya kukamatwa walipelekwa Dodoma mjini
kwa uchunguzi zaidi kutokana na tukio hilo.
Baada ya kufanyika jitihada
wakiwa katika kituo cha Bahi na kwa kuhofia kwamba kitendo cha kuendelea
kumkamata mwandishi wa habari kingeleta kelele nyingi mwandishi huyo aliachiwa
na kubakizwa Mtetezi wa Haki za Binadamu BB Dominic na wananchi hao sita. Mpaka
sasa wahusika bado wako kizuizini na hawana msaada wowote na kwa taarifa
tulizonazo wamebambikiziwa kesi nyingine ya kujeruhi.
RAI YETU
•
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
haujaridhishwa na mazingira ya kukamatwa kwa mwanachama wake na wananchi
waliotajwa kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, kila mwananchi anahaki ya
kupata taarifa sahihi za mapato na matumizi ya serikali katika ngazi zote ikiwa
ni pamoja na vijiji halmashauri za wilaya na serikali kuu. Lengo likiwa ni
kuzingatia uwazi ambayo ni nguzo muhimu katika kulinda utawala bora.
•
Tunalitaka Jeshi la polisi Mkoani Dodoma na
Wilayani Bahi watimize majukumu yao
kisheria na kuacha kutumika na baadhi ya viongozi was serikali wasiojua misingi
ya utawala bora na haki za binadamu.
•
Mtandao wa Watetezi unalitaka Jeshi la Polisi
kuwaachia huru watetezi hao kwani makosa waliyotuhumiwa kwa malengo ya
kuwaridhisha watawala katika eneo la Bahi yanaruhusu dhamana.
•
Tunawataka viongozi wote wa serikali wenye nia
mbaya dhidi ya watetezi wa haki za binadamu hapa nchini kuacha mara moja
kutumia vyombo vya dola kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu. .
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Board
of Directors:
Dr.
Helen Kijo Bisimba, Kharous Mpatani, Martina Kabisama, Tike Mwaipabipile,
Joseph Parsambei,
Saed
Kubenea, Hamisa Mmanga and Ernest Kimaya.
•
Pia Mtandao unawasihi viongozi wote waheshimu
kazi za waandishi wa habari kwani kitendo cha Afisa Mtendaji wa Kata kumpiga
ngumi mwandishi wa habari na kukanyaga kitambulisho chake ni kunyume na utawala
bora na kuingilia uhuru wa habari.
Onesmo Olengurumwa
MRATIBU MTANDAO WA
WATETEZI WA HAKI ZA
BINADAMU.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Board
of Directors:
Dr. Helen
Kijo Bisimba, Kharous Mpatani, Martina Kabisama, Tike Mwaipabipile, Joseph
Parsambei,
Saed
Kubenea, Hamisa Mmanga and Ernest Kimaya.
Post a Comment