Kocha mtarajiwa na anayetajwa kurudi katika klabu ya Chelsea mwezi wa saba, Jose Mourinho amesikika akitanabaisha ya kwamba angependelea kuwaona wachezaji wawili wakongwe wa klabu hiyo, Frank Lampard 34 na John Terry mwenye miaka 32 wakibakia katika timu hiyo.
Itakumbukwa ya kwamba wakati wa ukocha wake akiwa na timu hiyo Mourinho almaarufu kama "The Special One" alifanikiwa kupata mafanikio makubwa akiwa kama mengi kuliko kocha mwingine yule aliyewahi kuingoza timu hiyo. Mourinho alifanikiwa kuchukua makombe 2 ya Ligi kuu, makombe 2 ya FA and makombe matatu ya kombe la Ligi (League Cups), mbali na kuwahitaji wakongwe hao pia Mourinho anawahitaji wachezaji Ramadel Falcao kutoka kwa mahasimu wake wakuu wa sasa timu ya Athletico Madrid na Xavi Alonso kutoka timu yake ya sasa ya Real Madrid.
Itakumbukwa usiku wa Alhamisi mara baada ya timu ya Chelsea kufanikiwa kuingia fainali ya kombe la Europa mashabiki wa Chelsea waliliibuka tena na jina Mourinho tena na hii inaonyesha ni kwa jinsi gani kocha huyu anayopendwa Stamford Bridge.

Mourinho enzi ya utawala wake akiwa na wakongwe wa klabu hiyo kwa sasa Frank and John.
Je kwani Mashabiki wa Timu ya Chelsea hawamsahau Mourinho?????
NOTABLE
CHELSEA MANAGERS, BY WIN PERCENTAGE
|




Jose akiwa Jukwaani kwenye mchezo baina yao na Borrusia, sura inaonyesha siku zake zinakaribia ukingoni na Real Madrid

Mashabiki wakichangamkia medali ya ushindi ya Jose aliyowarushia mara baada ya kushinda taji la Ligi kuu ya Uingereza.

Post a Comment