Askari
polisi wasio waaminifu wameendelea na tabia ya kuwabambikizia kesi watu
hasa wafanya biashara mbalimbali katika maeneo ya kawe.
Askari
hao ambao kushirikiana na baadhi ya matapeli na kumfuata mtu na
kumuelezea matatizo kama vile kufiwa, kuuguliwa na mgonjwa na kuomba
msaada wa kiasi Fulani cha pesa pamoja na dhamana kama simu, komputa,
redio, luninga na kadhalika.
Katika
utapeli huo wa baadhi ya Polisi na matapeli hao pindi mtu anapoonyesha
dalili ya kutokuamini kuja na vitu hivyo kama mdhamana wa kupewa msaada
wa kifedha.
Akizugumzia
tukio hilo mmoja wa waathrika (jina tunalo) alisema baada ya muda au
siku moja kurudi tena akiwa amekamatwa na polisi na kwa madai kwamba
vitu alivyoweka kama dhamana vilikuwa ni mali ya wizi
Baada
ya songombigo hilo Polisi wanachukua uamuzi wa kuwakamata wote pamoja
kwa madai ya kukutwa na vitu vya wizi na kupelekwa kituoni.
Baada
ya kufika kituoni utaambiwa kuwa Yule mtu aliyekupa ule mzigo
anaendelea kuonyesha sehemu nyingine alikopeleka mali nyingine na wewe
utawekwa ndani kwa ajili ya kupelekwa mahakamani ukaunganishwe na
wenzako waliouziwa au kupewa mali za wizi.
Baada ya hapo ndipo hudai kiasi kikubwa chja pesa kati ya shilingi laki tano (500000)- milioni moja (1000000) ili waweze kukuachi huru
Ni
watu wengi sana wamekumbana na utapeli huu ambao hufanywa na askari wa
jeshi la polisi ambao sio waminifu na kuendelea kulitia doa jeshi la
polisi nchini
Post a Comment